Ligi Kuu

Moto wa Kariakoo Derby kupigwa Juni 15

DAR ES SALAAM:BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imetoa ratiba mpya ya mechi zilizobakia za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB, huku ikitangaza mabadiliko muhimu kwenye kalenda ya mashindano hayo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kati ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba SC, sasa umepangwa kuchezwa tarehe 15 Juni saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo huo umekuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa kutokana na ushindani mkali baina ya timu hizo msimu huu. Ligi hiyo sasa itahitimishwa rasmi Juni 22, badala ya Mei 25 kama ilivyopangwa awali.

Mabadiliko hayo yamesababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi pamoja na ratiba za kimataifa, ikiwemo mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na RS Berkane utakaochezwa Mei 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho la CRDB, fainali inatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 26 hadi 28. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona timu zipi zitafika hatua hiyo ya mwisho na kutwaa taji hilo la heshima.

Mabadiliko haya yanatoa nafasi kwa maandalizi bora ya timu, huku mashabiki wakitarajia burudani ya kiwango cha juu kutoka kwa vigogo wa soka la Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button