Burudani

Mr. Mwanya aendeleza utani mjini

DAR ES SALAAM: MUIMBAJI na mchekeshaji maarufu mjini, Mr Mwanya, anayevuma kwa misemo yake kama Shubamiti, Sakafyuka, Mwajuma Nyaugoko, Mwanaidi Kishepu Mshumaa, na Tatu Kiuno, ameendelea kufurahisha mashabiki wake kwa utani na maudhui ya kuvutia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mr Mwanya amechapisha ujumbe ulioibua mjadala mkubwa mitandaoni. Ameandika:
“Kuna mdada ata awe na njaa ya siku mbili, kidume uende na milioni zako tano ulale nae usiku mmoja tu, hakubali… huyo ndio mwanamke wa shoka sasa.”

Akimaanisha kuwa bado wapo wanawake waaminifu ambao hawakubali kushawishika kwa pesa, licha ya hali ngumu wanayoweza kuwa nayo.

Mr Mwanya hakusita kumalizia ujumbe wake kwa utani mzito aliposema:
“Mkinipiga makwenzi nawatajia wanapopatikana,”
na akaambatanisha na emoji za kucheka, akionesha kuwa alikuwa akizungumza kwa mtindo wake wa kawaida wa vichekesho.

Kupitia ujumbe huo, Mwanya aligusa suala la kuaminiana kwenye mahusiano, akielezea jinsi ambavyo siku hizi uaminifu umekuwa adimu, huku tamaa na kutokuridhika vikiharibu mahusiano mengi.

Kwa upande wa muziki, Mr Mwanya anafahamika kwa vibao kadhaa kama Safari ya Beach, Pombe, Nimefanikiwa, na Ex.
Swali linaibuka kwa mashabiki wake: Je, Mr Mwanya anapanga kutoa kazi mpya hivi karibuni?

Related Articles

Back to top button