Mastaa

Baada ya Jennifer Lopez wazazi wamtaka Ben Affleck achumbie tena

LOS ANGELES: WAZAZI wa mcheza filamu Ben Affleck wamemtaka kijana wao Ben Affleck achumbie tena mwanamke mwingine baada ya kuachana na Jennifer Lopez.
Ben Affleck anayetamba na filamu ya ‘Deepwater’ alimwelezea Jennifer Lopez alipokuwa akitokea kwenye Morning Joe ya MSNBC ili kutangaza filamu yake ijayo ya ‘The Accountant 2’: alisema “Watu unaowapenda zaidi ndiyo wanakupa wazimu zaidi,”.

Wanandoa hao walirudiana kwa mara ya pili baada ya uchumba wao mwanzoni mwa miaka ya 2000 kuyumba na kuanza kuonesha dalili za matatizo wakati wa kurekodiwa kwa mradi wao wa ‘This Is Me… Now: A Love Story’.

Wakati wa filamu ya ‘The Greatest Love Story’, Lopez aliangua kilio kutokutokea, akisema alijisikia mwenye hatia kwa kukosa tukio lililopangwa na Ben Affleck, kulingana na ripoti ya Daily Mail.

Wiki iliyopita Affleck alimwita Lopez mtu mzuri. “Kwa rekodi, Jennifer Lopez ni wa kuvutia, mzuri kwa watoto wangu, ni mtu muhimu sana, mtu wa uadilifu sana ambaye ninampenda na ninamshukuru kwa yote.”

Daily Mail iliripoti zaidi kwamba Luciana Barroso, mke wa rafiki mkubwa wa Affleck Matt Damon, amekuwa akimsihi aingie tena kwenye uchumba.

Lakini Affleck, ambaye amepambana na uraibu wa pombe amepitia hatua nyingi katika vituo vya kulea wanaotumia dawa za kulevya. “Familia yake pia inamhimiza awe na mchumba ikidai mwanamke anayekunywa pombe hamfai.

Baba huyo wa watoto watatu amesema katika mahojiano hayohayo, “Mimi ni mtu mwenye furaha kikweli kwa sasa.”

Related Articles

Back to top button