Onesho la vichekesho Kenya lauza tiketi zote

KENYA: KATIKA hali ya kushangaza tiketi za onyesho la ‘Let Me Explain’, uliofanyika katika Ukumbi wa Kitaifa wa Kenya ambalo liliandaliwa na mchekeshaji wa Kenya Mulamwah lilifanikiwa kuuza tiketi zote za onesho hilo kabla halijaanza.
Onesho hilo lilifanyika Aprili 20. Taarifa zinaeleza kuwa hali hiyo ya kustaajabisha imewashangaza wadau wa sanaa ya uchkeshaji huku wengi wao wakifurahia ukuaji wa sanaa hiyo ya uchekeshaji nchini Kenya.
Onyesho hilo liliungwa mkono na watumbuizaji wenzao akiwemo YY Comedian, Mcheshi Butita, Nana Owiti, Vinnie Baite, Arrow Bwoy, na Iyaani licha ya madai fulani mtandaoni kwamba mahudhurio ya watu mashuhuri yalikuwa machache lakini onesho limefanikiwa kwa kumaliza tiketi.
Maisha ya kibinafsi ya Mulamwah pia yalikuwa yanaangaziwa siku chache kabla ya onyesho. Muda mfupi kabla ya onyesho hilo, alithibitisha kupitia Facebook kwamba yeye na mpenzi wake wa muda mrefu Ruth K walikuwa wameachana ingawa baadhi ya mashabiki mtandaoni wanadai jambo hilo lilifanywa kama kick ili kufanikisha watu wengi kununua tikiti za onesho hilo.
Alisisitiza kwamba ikiwa kweli angetumia talaka kama njia ya kuongeza mauzo ya tikiti, angekuwa ameshindwa, kutokana na athari ya kihisia zinazotawala kwa sasa: “Nimechoka kutrend, mtu mwingine ajitokeze atrend maana naonekana nimetoa talaka ili kupata huruma ya mauzo ya tikiti kwa nini nifanye hivyo”.
Ili kuondokana na minongono ya mtandaoni mchekeshaji huyo Mulamwah leo April 24 ameweka picha ya mwanamke mnene, asiyejulikana akinukuu: “Kwa maisha mapya” akiwema emoj ya moyo. Picha hiyo ikionyesha mgongo wazi na kiuno cha mwanamke huyo ilizua hisia nyingi mtandaoni, huku mashabiki wakihoji uenda akawa mpenzi wake mpya baada ya kuachana na Ruth.