Muziki

Harmonize amtambulisha meneja wake wa Kimataifa

DAR ES SALAAM: MSANII Rajabu Abdul maarufu Harmonize amemtangaza aliyekuwa mtayarishaji mkuu wa wimbo wa ‘Single Again’ uliotayarishwa na DJ Tarico, Geobek Beke kuwa Meneja wake wa Kimataifa.

Geobek anajiunga na Harmonize kama Meneja wa Kimataifa na atasaidia timu ya Msanii huyo kwa ujuzi wake wa biashara ya muziki, ujuzi wa utayarishaji muziki na mkakati wa kupeleka kazi ya Harmonize ngazi za kimataifa.

George ni mtaalamu wa tasnia ya muziki na Mkurugenzi Mkuu wa Geobek Entertainment, kampuni inayoongoza katika tasnia ya muziki ya Kiafrika ambayo inashughulikia masuala mbalimbali ya muziki, vipaji, burudani na ufumbuzi wa vyombo vya habari.

Beke pia ni mshauri wa wabunifu chipukizi, akiwasaidia kukuza ujuzi wao, mitandaon, na kufikia hadhira ya juu. Ana shahada ya BA katika Mawasiliano ya Sauti na Picha kutoka Chuo Kikuu cha Johannesburg, ambapo aliboresha ujuzi wake katika utayarishaji wa vyombo vya habari na usimamizi wa kimkakati.

Beke amefanya kazi na wasanii mashuhuri kama vile Burna Boy, Mr Eazi, French Montana, Runtown, Harmonize, DJ Tarico na wengine wengi.

Related Articles

Back to top button