Clara Luvanga kinara wa mabao Al Nassr

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia Clara Luvanga ndiye kinara wa mabao katika timu yake baada ya kufunga jumla ya mabao 15.
Tayari timu yake ilishatangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo hivi karibuni wakiwa na mechi kadhaa mkononi.
Timu yake imebakisha michezo miwili kumaliza msimu huku Clara akiwa amefunga jumla ya mabao 15.
Bado anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wachezaji wenzake wa Al Nassr wakiwemo Maria Eduarda raia wa Brazil mwenye mabao 13 huku Lina Boussaha wa Algeria akiwa na 11.
Kwa ujumla katika ligi, Clara anashika nafasi ya nne huku kinara akiwa ni Ajara Nchout wa Al-Qadsiah mwenye mabao 24, Ibtissam Jraid wa Al-Ahli mabao 22 na Naomie Kabakaba wa Al-Ahli akiwa na 21.