Mastaa

Ali Baba: Nimewafuma wake wa rafiki zangu wakitoka na magavana

GHANA: MCHEKESHAJI mkongwe wa Nigeria, Ali Baba, amefichua kuwa amewanasa wake wengi wa marafiki zake na washirika wake wakijihusisha na mapenzi nje ya ndoa.

Ali Baba amesema wanawake hao wengi wao amewaona wakitoka na baadhi ya magavana na wanasiasa matajiri wa nchini humo bila kujali ndoa zao.

Ali Baba alitoa ushuhuda huo alipokuwa akihojiwa katika podcast moja nchini humo.

Akizungumza kwa uwazi kuhusu Sakata hilo mchekeshaji huyo alisema alimwona mke wa mshirika wake katika makao ya gavana wa jimbo moja wapo nchini Ghana.

Alisema: “Nimekuwa katika nyumba za watu wengi wakubwa za magavana na matajiri wakubwa nchini Ghana huko nimeona wake za watu wengi ninaowajua wakifanya mambo ya hovyo bila kujali ndoa zao na nilikuwa nikiwasalimu, ‘Habari zenu”

“Wengine walijibu kwa hofu wakiwaambia wanaume hao warudi ndani kwa kuwa hawajamalizana nao. ‘Rudi ndani, sijamalizana na wewe,’ na wanaume hao ‘wanarudi ndani.

Ali Baba amesema cha kushangaza ni kuwa wanawake hao alipowakuta na wanaume wao waliowaoa walitambulishwa kwao, “Habari yako? Kutana na mke wangu.” Nikawajibu! ‘Oh madam, ni furaha kwangu’.

“Anaponiona mahali fulani baadaye, ananiita na kusema, ‘Ali, asante akimaanisha sijamuumbua mbele ya mume wake,’ nasema, ‘Sawa.’”

Kauli ya muigizaji huyo Ali Baba inawataka wanawae waliokwenye ndioa kuheshimu ndoa zao nak ama wanafuata maslai wasiingie katika ndoa na wanaume wasio na maslai nao kwa sababu wanaweza kuhatarisha usalama wao pindi watakapojulikana usaliti wao.

Related Articles

Back to top button