Mastaa

Lulu Diva ajitamba kuwa fundi wa mapishi

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’, amefichua siri yake ya upishi, akidai kuwa hakuna staa anayeweza kumfikia katika sanaa hiyo.

Akizungumza na Spotileo katika tukio la Usiku wa Huba Gala, msanii huyo alisema kuwa kama angeamua kufanya biashara ya upishi, basi hakuna mtu ambaye angeweza kupinga ladha ya chakula chake.

“Napika sana! Yaani ni fundi haswa, asikwambie mtu. Achana na hao wengine wanapika pika tu, lakini mimi napika hatari,” amesema Lulu Diva kwa kujiamini.

Mbali na hilo, msanii huyo pia alizungumzia suala la watu kulalamika kuhusu mastaa kufuturishwa, akisema kuwa si kila mtu mwenye umaarufu hana changamoto za maisha.

“Si kwa kuwa mtu ni maarufu ndiyo hastahili kufuturishwa. Na yeye ana haki kama wengine, anaweza kuwa na shida lakini wewe hujui. Kuvaa vizuri na kupendeza si kigezo cha kutokuwa na matatizo,” aliongeza Lulu Diva.

Related Articles

Back to top button