Kwingineko

Newcastle yamponza Gravenberch

ROTTERDAM, Sasa ni rasmi kuwa Kiungo wa majogoo wa jiji Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Ryan Gravenberch ataukosa mchezo wa timu yake ya taifa wa robo fainali ya Mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League) dhidi ya Hispania baada ya kupata majeraha akiitumikia Liverpool.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini humo limemnukuu kocha mkuu wa kikosi hicho kuwa kukosekana kwa kiungo huyo kutafifisha nafasi yao lakini sio tatizo kwakuwa Memphis Depay na Frenkie de Jong wako fiti kwa mchezo huo utakaopigwa leo saa 4:45 usiku katika uwanja wa Stadion Feijenoord jijini Rotterdam.

“Ryan Gravenberch ameondoka kambini jana jioni, kiungo wetu huyu bado anasumbuliwa na majeraha aliyopata wikiendi iliyopita na bila shaka hatacheza dhidi ya spain” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kiungo huyo mwenye miaka 22 aliumia katika kichapo walichopata Liverpool Jumapili kutoka kwa Newcastle United katika fainali ya kombe la Carabao. Msimu huu Gravenberch ameanza katika kikosi cha kwanza cha Arne Slot na atakuwa chini ya uangalizi kuelekea mchezo wa Merseyside Derby Aprili 2

Related Articles

Back to top button