Ligi KuuNyumbani

Kirumba, Uhuru kuwaka moto ligi kuu leo

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili Dar es Salaam na Mwanza.

Katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam KMC ni mwenyeji wa Mtibwa Sugar wakati Ruvu Shooting imesafiri hadi Kanda ya Ziwa kuikabili Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mtibwa Sugar inashika nafasi 7 katika msimamo wa ligi ikiwa pointi 9 baada ya michezo 6 wakati KMC ipo nafasi ya 11 ikiwa pointi 7 baada ya michezo 6.

Kwa mara mwisho timu hizo zilipokutana katika mchezo wa ligi Mei 12, 2022 KMC iliifunga Mtibwa Sugar mabao 3-2.

Nayo Ruvu Shooting inashika nafasi 5 ikiwa na pointi 10 baada ya michezo 7 wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 6.

Timu hizo zilitoka suluhu zilipokutana kwa mara ya mwisho katika mchezo wa Ligi Kuu Mei 21, 2022.

Related Articles

Back to top button