Mawimbi, upepo vyakata Trace Awards Zanzibar

ZANZIBAR, Tuzo za Trace zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Visiwani Zanzibar zilikatishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo upepo mkali na mawimbi makubwa yaliyosababisha maji kujaa karibu na jukwaa.
Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa wanamuziki wa Kiafrika waliofanya vizuri zaidi barani humu zilizoonekana kuchelewa kuanza kutokana na uwepo wa upepo mkali na mawimbi hali iliyowalazimu waandaaji kusogeza mbele muda wa kuanza kwa tuzo hizo hadi saa 4 usiku badala ya saa 2 usiku kama ilivyokusudiwa awali.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tamasha hilo lililoanza kwa wasanii mbalimbali kuburudisha na lilikatishwa mishale ya saa 9:20 usiku, likiwa katika hatua za mwanzo za kutangaza baadhi ya washiriki wa categories mbalimbali za tuzo hizo.
Baadhi ya tuzo zilizotoka kabla ya kukatishwa kwa Trace Awards ni pamoja na ile ya msanii bora wa kiume wa mwaka pamoja na album bora ambazo zimeenda kwa Rema kutoka Nigeria, producer bora akitwaa P.Priime wa Nigeria, msanii bora wa nchi zinazozungumza kifaransa akishinda Josey kutoka Ivory Coast, Joe Dwet File akishinda tuzo ya msanii bora kwa upande wa diaspora (Ulaya). Kwa upande wa diaspora wa Brazil ameshinda msanii Duquesa.
Tuzo hizo zimefanyika kwa mara ya kwanza hapa Tanzania, huku ikishuhudiwa performances kutoka kwa wasanii wengi wakubwa kama Fally Ipupa, Qing Madi, Diamond, huku Harmonize na Bien kutoka Kenya, wakiwakosha wengi kwa uwezo wao mkubwa jukwaani.



