EPL

Haaland hatihati kuikosa Liverpool

MANCHESTER, Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika na upatikanaji wa mshambuliaji wake kinara Erling Haaland kwenye mchezo dhidi ya Liverpool Jumapili baada ya kukosekana kwenye kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Jumatano.

Haaland aliukosa mchezo huo baada ya kutolewa dakika za mwisho katika mchezo ambao vijana hao wa Guardiola walishinda 4-0 dhidi ya Newcastle United kwa kile kinachotajwa kuwa ni jeraha la goti.

“Sijui kama atakuwepo, labda kesho tutajua. Unajua ni vizuri kuwa na Erling mchezoni, kila mtu anahusika na kila zuri tunalopata lakini kuwa na Erling kikosini ni bora zaidi” – Guardiola amewaambia waandishi wa habari.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya England wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi Liverpool katika michezo 15 ambayo wamekuwa wenyeji kwenye dimba la Etihad.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button