Haaland: Mashabiki tuvumilieni

MADRID, Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amewaangukia mashabiki wa timu hiyo na kuwaomba wawe watulivu na wawaunge mkono katika kipindi hiki ambacho timu hiyo inapitia wakati mgumu.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Erling Haaland pia amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa uungwaji mkono na kuwaomba wawe wavumilivu huku wakiahidi kujitoa zaidi kuhakikisha timu hiyo inarejea kwenye makali yake.
“Tunaendelea kubaki pamoja, wakati mwingine ni lazima upitie changamoto kama hizi kwenye maisha na ujifunze kutokana nazo, huwezi kushida muda wote. Tutasimama tena pamoja” Ameandika Erling Haaland kwenye Instagram.
Manchester City wameondolewa kwenye hatua ya mtoano ya kuwania kucheza hatua ya 16 bora kwa jumla ya mabao 6-3 yaliyopatikana katika michezo miwili ya hatua dhidi ya Real Madrid.