Africa

Simba ya 11 Afrika, 130 duniani

KLABU ya soka ya Simba ni miongoni mwa klabu 20 bora barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Kimataifa la Takwimu na Historia ya soka takwimu(IFFHS) iliyotolewa leo, Simba inashika nafasi ya 11 Afrika na ya 130 duniani na takwimu hizo zimetokana na matokeo ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.

Akizungumza na Spotileo, Menyekiti wa timu hiyo Murtaza Mangungu amesema takwimu hizo zimewatia moyo viongozi na wawekezaji na kuwaongezea nguvu ya mapambano ili kutimiza lengo la kuifanya Simba kushika nafasi za juu zaidi.

“Kwa takwimu hizi zinathibitisha kwamba kuna kitu tumekifanya ndio maana ni klabu ya pekee Tanzania ambayo inaongoza kwa mafanikio kwenye michuano ya kimataifa na tumejiwekea viwango vyetu ili kufika tulipo pakusudia,” amesema Mangungu.

Katika mechi za nyumbani kwa maana ya ligi Simba imekuwa katika kiwango bora kwani ni miongoni mwa timu tatu ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Kwa sasa Simba ipo juu ya klabu za TP Mazembe, AS Vita zote za Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo, Esperance ya Tunisia, ES Setiff ya Algeria na nyingine zilizotamba miaka ya nyuma.

Related Articles

Back to top button