Ligi Kuu

Yanga: Kagera njooni mchana, njooni usiku

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Yanga kimeanza kupiga hesabu kali kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, kikizitaka alama zote tatu katika Mchezo unatarajiwa kuchezwa kesho kutwa Uwanja wa KMC, Complex, mwenge jijini Dar.

Kocha wa Yanga Sead Ramovic amedai ushindi katika mchezo huo ni lazima ili kutengeneza mazingira ya kutetea ubingwa wao ambao wameuchukua kwa misimu mitatu mfululizo.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison amesema anaamini kikosi chao kitapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo na kuzidi kutengeneza mazingira ya kutetea ubingwa wao ambao wameuchukua msimu uliopita.

“Maandalizi yanaendelea vizuri ukizingatia kuwa msimu huu tunataka kuendelea tulipoishia kusaka mataji yote ya ndani, mechi zipo nyingi ambapo kila mchezaji atapata nafasi ya kusaidia timu kufikia malengo. Jambo la kushukuru ni kwamba, Wachezaji wapo katika hali nzuri isipokuwa Yao Kouassi ambaye anaendelea kuuguza majeraha, kikubwa mashabiki wetu wajiandae kuja Uwanja wa KMC Complex ili kupata burudani ya kutosha,” amesema.

Walter amesema hawauchukulii mchezo wowote kwa masihara na badala yake watahakikisha wanapata matokeo mazuri kwani malengo waliyonayo kwa sasa ni kushinda michezo yote ya mzunguko huu wa pili.

“Huu mzunguko wa pili hatutakiwi kupoteza, tunatakiwa kuwa makini kutafuta matokeo ambayo yatatufanya kurejea kwenye nafasi yetu ya kuongoza ligi. Tunajua kazi haitakuwa rahisi ndio maana tunaendelea kufanya maandalizi ya nguvu,” amesema.

Walter amesema kutokana na hali ya wachezaji hao kuwa imara suala la mabadiliko ya kikosi yatakuwa chini ya kocha wao Saed Ramovic kulingana na aina ya wapinzani wanaokwenda kukutana nao.

Related Articles

Back to top button