Kwingineko

Gvardiol aitetea Man City UCL

MANCHESTER: Beki wa kushoto wa Manchester city Josko Gvardiol amesema kufanya vibaya kwa klabu yake katika ligi ya mabingwa barani Ulaya kunatokana na wao kuwekeza zaidi nguvu zao kwenye ligi kuu ya England.

Gvardiol ameiambia TNT sports kuwa kutokana na hali mbaya ya kikosi hicho iliwalazimu kuchagua eneo moja la kuweka nguvu zao na wao waliona ligi kuu ya England kama sehemu sahihi.

“Tulikuwa na hali mbaya, labda hatukufikiria mapema kukusanya pointi kwenye ligi ya mabingwa, tulijikita zaidi kwenye Ligi, na sasa tuko kwenye hali ambayo tunatafuta kujinasua, nina hakika tunaweza.” amesema Gvardiol

Manchester city wanashika nafasi ya 25 kwenye msimamo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya na pointi 8 wakishinda mechi 2, droo 2 na kupoteza 3. Huku wakihitaji point 3 kutoka Club Brugge ili wasiondolewe moja kwa moja kwenye michuano hiyo inayochezwa kwa mfumo wa ligi

Related Articles

Back to top button