Kwingineko

Charles Mmombwa mambo safi Australia

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Charles M’mombwa amejiunga na klabu ya Newcastle United Jets inayoshiriki Ligi kuu Australia.Mmombwa kabla ya kujiunga na Newcastle alikuwa anaitumikia Macarthur FC ya nchini Australia.

Klabu yake hiyo mpya imemtambulisha na kukamkaribisha tayari kuwatumikia kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Karibu Charles M’mombwa, mchezaji wa kimataifa wa Tanzania,”ilisema taarifa hiyo ambayo pia, mchezaji huyo alijibu kwa ishara ya mikono kushukuru.

Katika msimamo wa Ligi Kuu ya Australia,Newcastle Jets haiko katika nafasi nzuri, inashika nafasi ya 11 yaani nafasi ya tatu kutoka chini ikiwa na pointi 10 ilizovuna kwenye michezo 12.

Usajili wa M’mombwa huenda ukaleta matumaini katika kuisaidia kufanya vizuri na kujiondoa nafasi za chini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button