Africa

Simba kuifuata De Agosto Oktoba 6

Msafara wa klabu ya soka ya Simba unatarajiwa kwenda Angola Oktoba 6 kwa ajili ya mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Primeiro De Agosto ya Angola.

Akizungumza na Spotileo, Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu amesema maandalizi ya timu hiyo yanakwenda vizuri kuelekea mchezo huo.

“Tunatarajia kuondoka Alhamisi kuwafuata De Agosto ni mchezo mgumu lakini tunakwenda na tahadhari zote sababu lengo letu ni kushinda ugenini ili mchezo wa marudiano tutakaocheza nyumbani tuwe na kazi nyepesi,” amesema Rweyemamu.

Kwa mujibu Rweyemamu wachezaji wote wapo katika hali nzuri na benchi la ufundi tayari limeshaanza kuwafuatilia wapinzani wao De Agosto.

Simba itacheza na De Agosto Oktoba 9 nchini Angola marudiano yakifanyika Tanzania Oktoba 16.

Related Articles

Back to top button