BurudaniMuziki

Zuchu, Adenkule wana jambo lao

MWANAMUZIKI nyota, Zuhura Othman ‘Zuchu’ ameweka wazi kuwa miongoni mwa nyimbo mbili atakazoachia wiki hii, moja inaitwa Love aliyomshirikisha mkali wa muziki wa Nigeria, Adekunle Kosoko ‘Adenkule Gold’.

Akizungumza na gazeti la HabariLEO Dar es Salaam, Zuchu amesema mbali na hiyo atakayoitoa rasmi Ijumaa hii, wimbo mwingine ameahidi kuuachia hewani Oktoba 4, mwaka huu alioupa jina la Kwikwi huku akiwasisitiza mashabiki zake wakae tayari kufurahia kazi zake
hizo.

Huo ni mwendelezo wa Zuchu kutimiza ahadi yake aliyoitoa takribani siku 10 zilizopita juu ya ujio wa nyimbo zake hizo mbili ikiwa ni mara ya tatu sasa anafanya hivyo tangu alipoanza kutambulika miaka mitatu iliyopita.

Julai mwaka huu aliachia nyimbo mbili za Jaro na Fire. Pia Septemba, 2020 alitoa nyimbo
mbili kwa mpigo za Cheche na Litawachoma ambazo zilifanya vizuri.

Tayari mashabiki wengi wamevutiwa na wimbo alioshirikishwa Adenkule kutokana na ubora
alionao anapoimba nyimbo za mapenzi kama zile zilizovuma za Something Different, Before You Wake Up, Promise na nyingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button