Mastaa

Kesi ya Diddy hadi Mei 2025, Watoto wake wafika Mahakamani

NEW YORK: JAJI anayesimamia kesi ya rapa Sean Combs mwenye miaka 54 maarufu P.Diddy, Arun Subramanian amepanga kesi hiyo kuja mahakamani tena Mei 5, 2025 baada ya jana Oktoba 10, rapa huyo kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo Mama wa rapa huyo aliyetamba na wimbo wa ‘I’ll Be Missing You’ Jenice na watoto wa rapa huyo kutoka kwa mama tofauti Quincy (33), Justin (30), Christian (26), Chance (18), mapacha D’Lila na Jessie (17) na mtoto mdogo wa miazi 23 wanadaiwa kuonekana kwa mara ya kwanza katika Mahakamani wakishiriki siku ya kwanza ya P. Diddy kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi yake ikisomwa.

Hiyo imekuja siku moja tu kabla ya wakili wake Alexander A.E. Shapiro alipowasilisha makaratasi ya rufaa kwa Mahakama ya Rufaa ya Marekani kwa Mzunguko ya Pili akiomba Combs aachiliwe hadi kesi yake ya msingi itakapofikishwa mahakamani.

“P Diddy anaelezwa kwamba inachukuliwa kuwa haina hatia. Alisafiri hadi New York kujisalimisha kwa sababu alijua angefunguliwa mashtaka. Alichukua hatua za ajabu kuonyesha kwamba alikusudia kukabili na kupinga mashtaka, na sio kukimbia.

“Aliwasilisha kifurushi cha dhamana ambacho kingemzuia wazi kuwa hatari kwa mtu yeyote au kuwasiliana na mashahidi wowote. Chini ya Sheria ya Marekebisho ya Dhamana, ‘uhuru ni jambo la kawaida, na kuwekwa kizuizini kabla ya kusikilizwa kesi au bila kesi ni ubaguzi uliowekewa mipaka’.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 54 alikamatwa mjini New York mwezi uliopita na bado yuko korokoroni akisubiri kesi ya mashtaka ya ulanguzi wa ngono na ulaghai baada ya kunyimwa dhamana ya dola milioni 50 na kwa sasa anazuiliwa katika kizuizi cha Metropolitan cha Brooklyn.

Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka hayo Combs amekana mashtaka ya kula njama ya ulaghai, ulanguzi wa ngono kwa nguvu, ulaghai, au kulazimisha na usafirishaji pamoja na kushiriki katika ukahab

Related Articles

Back to top button