EPL

47 wajeruhiwa, wanne hali mbaya sherehe za Liverpool

LIVERPOOL:MEYA wa jiji la Liverpool nchini England Steve Rotheram amethibitisha kuwa watu wanne wanauguza majeraha mabaya hospitalini kufuatia mwanaume mmoja mwenye miaka 53 mkazi wa jiji hilo, kuendesha gari na kuwagonga mashabiki wa Liverpool wakati klabu hiyo ikiendelea na ‘parade’ la ubingwa wa 20 wa ligi kuu ya England.

Rotheram ameiambia BBC sport kuwa watu hao ni wale ambao video za tukio hilo zilionesha wakiwa chini ya uvungu wa gari hilo aina ya Ford galaxy ambalo pia mashabiki wenye hasira walilivamia na kulishambulia kwa magongo kabla ya dereva wake kuokolewa na polisi.

Tukio hilo lililotokea Jumatatu jioni katika mitaa ya katikati ya jiji la Liverpool ambayo ilifurika idadi ya watu wanakadiriwa kufika milioni moja limetajwa na polisi nchini humo kuwa ni tukio la kawaida la chuki za kishabiki na halihusiani kabisa na masuala ya ugaidi bila kutoa ushahidi wa kutosha kusapoti madai hayo.

Liverpool ilitwaa ubingwa wake wa mwisho kipindi cha COVID-19 kipindi ambacho sherehe zilikua zimepigwa marufuku hivyo ubingwa wa msimu huu ulivuta hisia za mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kusherehekea

Tukio hilo lilitokea kwenye mtaa wa Water ambao ulifungwa kuzuia magari ili kuruhusu mashabiki wa Liverpool kusherehekea ubingwa huo na kujeruhi mashabiki 47 wakiwemo watoto wawili na wengine wawili kupata majeraha makubwa eneo la tukio kabla ya idadi hiyo kufikia wanne asubuhi ya leo.

Related Articles

Back to top button