2Baba atangaza uongozi mpya katika muziki wake

NIGERIA: MWANAMUZIKI mashuhuri wa Nigeria Innocent Idibia maarufu 2Baba ametangaza timu mpya ya usimamizi wa kazi zake za muziki.
Nyota huyo wa Afrobeat ameandika habari hiyo kwenye Instagram, akisisitiza kwamba timu hiyo ilichaguliwa kufufua na kutathmini urithi wake katika tasnia ya burudani ya Afrika.
Katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari, timu ya 2Baba iliangazia mchango wake mkubwa kwenye eneo la muziki, ikibainisha kuwa msanii huyo anamchango mkubwa mno katika nchi hiyo hivyo anastahili kuwa na uongozi thabiti kwa ajili ya kusimamia kazi zake za kimuziki.
“Tunafuraha kutangaza rasmi sura kuu katika taaluma ya gwiji wa muziki wa Nigeria, Innocent Ujah Idibia, anayejulikana kama 2Baba. Timu ya usimamizi, iliyokusanywa kwa uangalifu ili kubuni upya na kukuza kila kipengele cha chapa ya 2Baba.
“Nimefurahishwa na sura hii mpya. Mabadiliko ni sehemu muhimu ya ukuaji, na ninaamini timu hii inaelewa maono yangu, urithi wangu, na tunakoelekea. Hatusherehekei tu yaliyopita, tunaunda mambo mapya zaidia ya mafanikio.” Ameeleza 2Baba.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa timu hiyo mpya inajumuisha wataalamu wa juu katika muziki, chapa na sheria za burudani. Walidumisha kujitolea kwa uhalisi na uwajibikaji wa kijamii.