EPL

Fabrizio Romano ampa Maguire maua yake

MANCHESTER:BEKI wa Manchester United, Harry Maguire, amepongezwa sana wiki hii baada ya kuibuka shujaa kwenye ushindi wa United wa 2-1 dhidi ya Liverpool pale Anfield, ushindi wao wa kwanza hapo tangu mwaka 2016.

Lakini kilichogusa wengi ni ujumbe wa Fabrizio Romano kupitia Instagram, akimtetea Maguire na kumpongeza kwa uvumilivu wake licha ya miaka ya mzigo wa lawama na mizaha juu yake mitandaoni.

Romano aliandika: “Harry hajawahi kulalamika, hajawahi kujibu matusi. Ameendelea kufanya kazi kwa bidii, akiamini ndoto yake ya kuchezea Manchester United.”

Mwandishi huyo mashuhuri amesema hadithi ya Maguire ni msukumo kwa watu wote wanaopitia changamoto kwamba ukibaki imara, ukifanya kazi kwa bidii na ukikataa kukata tamaa, “mambo mazuri yatakuja tu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button