EPL

Majeraha yakuna kichwa cha Ten Hag

MANCHESTER: KOCHA mkuu wa Manchester united Erik ten Hag atakutana na ugumu wa kupata kikosi cha kwanza pindi Ligi Kuu ya England itakaporejea kutokana na wingi wa majeruhi ndani ya kikosi cha the Red Devils.

Duru zinaeleza kuwa Luke shaw na tyrell Malacia wameonesha maendeleo makubwa kwenye majeraha yao lakini hawatarajiwi kuwa imara vya kutosha kuwavaa Brentford wikiendi hii ikimuongeza msongo wa mawazo Ten Hag ambaye amekuwa akihangaika na ‘fitness’ ya wawili hao tangu kuanza kwa msimu huu.

Beki wa kushoto Diogo Dalot na wa kulia Noussair Mazraoui wamekuwa nguzo ya United msimu huu, bahati mbaya Mazraoui anatarajiwa kukosa wiki kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa moyo na kumuacha Dalot kuwa chaguo la pekee kwa Ten Hag

Mashabiki wa Man United kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakililia kupewa nafasi kwa kinda mwenye umri wa miaka 17 wa Akademia ya klabu hiyo Harry Amass. Hata hivyo Ten Hag amekuwa akisisitiza kuwa kijana huyo hajakua kubeba majukumu ya timu ya wakubwa.

Manchester united wanashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England wakishinda mechi 2, sare 2 na vipigo 3. Wamefunga mabao 8 na kufungwa 10 baada ya mechi 7 walizocheza na Oktoba 19 watawakaribisha Brentford dimbani Old Trafford.

Related Articles

Back to top button