Filamu

Wasanii watakiwa kuongeza viwango vya filamu za Tanzania

DAR ES SALAAM: WADAU wa filamu nchini wamehimiza utengenezaji wa kazi zenye ubora na viwango vya kimataifa ili kukuza hadhi ya soko la filamu Tanzania na kuinua vipaji vipya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Munirah Pendeza, ‘Tusa’ ndani ya tamthilia hiyo, amesema sekta ya filamu kwa sasa imekuwa na hamasa, morali na motisha kubwa miongoni mwa watayarishaji, hivyo wasanii wanapaswa kufanya kazi kwa ubora zaidi ili kuendana na kasi hiyo.

Tusa amewahimiza mashabiki kutumia ofa maalumu ya msimu wa sikukuu kwa kulipia ving’amuzi vya StarTimes, ili kufurahia maudhui mbalimbali ikiwemo tamthilia ya Nice to Meet You, katuni za watoto kama Bonnie Bears (maarufu kama Kipara Mbabe), Super Wings, pamoja na maudhui ya michezo na tamthilia zilizotafsiriwa kwa Kiswahili.

Kwa upande mwingine, msanii Nyota Waziri amesema tamthilia hiyo imeandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu na inagusa maisha halisi, ikimuonyesha mume anayehusiana na wanawake wawili wanaohisi kupendwa zaidi kuliko wenzao.

“Utashuhudia pia mzazi anayempenda mtoto kupita kiasi hadi kumsahau mwenzi wake. Usikose kufuatilia msimu huu wa sikukuu,” amesema.

Naye Meneja wa StarTimes, David Malisa, alisema kampuni hiyo imezindua kampeni ya “Lipia Tukubusti” kwa wateja wa Dishi na Antenna, ambapo mteja anayelipia kifurushi cha mwezi mzima atapandishwa daraja hadi kifurushi cha juu bila malipo ya ziada kwa mwezi mzima.

“Lipia kifurushi cha nyota 11,000 na tunakubusti hadi Mambo17,000. Vifurushi vikubwa pia vimeongezewa siku tano,” amesema Malisa.

Related Articles

Back to top button