EPLKwinginekoLa Liga
Villa kumsajili Moreno kwa bil 37/-
KLABU ya Aston Villa imekubali dili la kumsajili beki wa kushoto wa Real Betis ya Hispania Alex Moreno kwa pauni milioni 13.2 sawa na sh bilioni 37.1.
Usajili wa mhispania huyo mwenye umeri wa miaka 29 ni wa kwanza wa kocha Unai Emery kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu England(EPL).
Moreno ambaye alihusishwa kuhamia Nottingham Forest msimu uliopita amecheza mechi zote isipokuwa moja za Betis Ligi kuu ya Hispania, La Liga hadi sasa msimu huu.
Anatarajiwa kufanyiwa vipimo saa 48 zijazo kabla kukamilisha taratibu za uhamisho.
Villa ipo nafasi ya 11 EPL na imeondoshwa katika michuano ya Kombe la FA mwisho wa wiki baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka klabu ya League 2, Stevenage.




