EuropaKwingineko

UEFA yamfungulia mashitaka Mourinho

MUUNGANO wa Vyama vya Soka barani Ulaya(UEFA) umemfungulia mashitaka Kocha Mkuu wa Roma, Jose Mourinho ukimtuhumu kutumia lugha isiyofaa dhidi ya mwamuzi baada ya fainali ya Ligi ya Europa Mei 30.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 60 alioneshwa kadi ya njano na mwamuzi Anthony Taylor wa England jijini Budapest, Hungary ambako Sevilla ya Hispania iliifunga Roma kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya sare ya 1-1 na kutwaa ubingwa.

Mashitaka hayo yanahusiana na tukio kwenye eneo la kuegesha magari nje ya uwanja baada ya mchezo wakati Mourinho alipoelekeza maneno yasiyofaa kwa Taylor.

Sevilla na Roma pia zimefunguliwa mashitaka kutokana na mashabiki kurusha vitu, kuwasha fataki na mwenendo usiofaa wa timu hizo.

Wakati wowote Bodi ya Udhibiti, Maadili na Nidhamu ya UEFA(CEDB) itatoa maamuzi kuhusu suala hilo.

Related Articles

Back to top button