Michezo Mingine
Twiga Stars yafuzu raundi ya pili Olimpiki

Timu ya soka ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” imefuzu kucheza raundi ya pili ya kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 baada ya Congo kujiondoa.
Baada ya Congo kujitoa Twiga Stars itacheza na Botswana mwezi Oktoba ikianzia nyumbani.
Michezo ya Olimpiki Paris 2024 imepangwa kuanza Ijumaa Julai 26 na kumalizika Jumapili Agosti 11, 2024 nchini Ufaransa.