Muziki
Tiwa Savage: Sina mpango wa kuacha muziki

ABUJA: Nyota wa muziki kutoka Nigeria Tiwa Savage amesema hana mpango wa kuacha muziki licha ya kuanzisha taasisi mpya ya kusaidia vipaji chipukizi barani Afrika.
Savage alisema wazo la kuanzisha taasisi hiyo lilitokana na uzoefu wake binafsi alipokuwa mwanafunzi wa ufadhili katika Berklee College of Music nchini Marekani.
Alieleza kuwa msaada alioupata wakati huo uliibadilisha kabisa mwelekeo wa maisha yake ya muziki na ulimsaidia kuelewa biashara ya muziki.
Kwa sasa, Tiwa Savage amesema anaona ni wakati muafaka kutumia uzoefu na ushawishi wake kuwasaidia wasanii chipukizi kupata fursa bora katika tasnia ya muziki barani Afrika.




