
TIMU 32 zimefuzu hatua inayofuata ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA.
Michezo ya hatua hiyo ya 32 bora itachezwa mwisho wa Januari 2023.
Timu zilizofuzu ni Copco, Mbuni, Gwambina, Green Warriors, Rhino Rangers, Polisi Katavi, Mbeya City, Azam, JKT Tanzania, Kengold, Mashujaa, Mapinduzi, New Dundee, African Sports, Nzega United na Geita Gold.
Nyingine ni Ihefu, Kagera Sugar, Dodoma Jiji, Ruvu Shooting, Coastal Union, Simba, Buhaya, Namungo, Polisi Tanzania, Mtibwa Sugar, Prisons, Singida Big Stars, KMC, Yanga, Pan Africans na Mbeya Kwanza.