Ligi Ya WanawakeNyumbani
Tiger Queens mdomoni mwa Simba Queens leo

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam na Iringa.
Simba Queens inayoongoza ligi hiyo itaikaribisha The Tiger Queens kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Nayo Baobao Queens itakuwa mgeni wa Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa.