AFCONAfrica

U20 wanaume dimbani leo

TIMU ya soka ya taifa ya wanaume chini ya miaka 20 leo inaanza kampeni kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) U20 kanda ya Baraza la Vyama vya soka Mashariki na Kusini mwa Afrika(CECAFA) dhidi ya Uganda.

Mchezo huo wa kundi B utafanyika saa 1 usiku katika uwanja wa Al Hilal, Sudan.

Katika mechi mbili za ufunguzi kundi A Oktoba 28 Burundi imeichapa Djibouti mabao 5-0 wakati Sudan na Sudan Kusini zimetoka suluhu.

Finali za AFCON U20 zitafanyika Misri 2023.

Related Articles

Back to top button