Kwingineko

Steve Nyerere: Daraja la jamii na mwana-Harakati wa maendeleo

DA R ES SALAAM: MWENYEKITI wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steven Waiton Mengele, maarufu kama Steve Nyerere, ni miongoni mwa wadau muhimu wa maendeleo nchini kupitia mchango wake mkubwa katika sanaa za maigizo na uchekeshaji kwa miaka mingi.

Kwa muda mrefu, Steve ameendelea kuwa nguzo kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji, wasanii na wadau wa sanaa kwa ujumla, akihakikisha anakuwa daraja la kusaidia na kuunganisha watu wanaohitaji msaada kwa namna moja au nyingine.

Kupitia jitihada zake binafsi pamoja na ushirikiano kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya nchi, amefanikiwa kupunguza au kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu aliofikiwa.

Rekodi zinaonesha kuwa Steve amekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa misaada ya hali na mali kwa watu wengi, hususan pale ambapo jambo liko ndani ya uwezo wake kulishughulikia.

Nia yake thabiti ya kuleta mabadiliko chanya imeendelea kumjengea uaminifu mkubwa kutoka kwa taasisi, viongozi, wadau na jamii, kiasi cha kutazamwa kama daraja muhimu linalowaunganisha Watanzania walio na uhitaji.

Kutokana na utendaji wake, Steve Nyerere amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii, sio tu kwa namna anavyoratibu na kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii, bali pia kwa namna anavyotumia nafasi yake kusambaza ujumbe muhimu pindi inapobidi kufanya hivyo kwa maslahi ya umma.

Related Articles

Back to top button