Stanisic ajutia kumsukuma ball boy

MILAN, BEKI wa vinara wa Bundesliga Bayern Munich Josip Stanisic amesema kitendo alichofanya cha kumsukuma muokota mipira katika uwanja wa San Siro jana wakati wa mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya wenyeji Inter Milan kilikuwa ni cha ‘Kipumbavu’
Wajerumani hao walikuwa wakisaka goli la dakika za lala salama wakati beki huyo alipojaribu kurusha haraka mpira uliokuwa umetoka nje ya mchezo, mpira ambao muokota mipira (ball boy) alijaribu kuusogeza mbali kitendo kilichompandisha hasira Stanisic na kuamua kumsukuma na kumuangusha ball boy.
Akizungumza na gazeti la Kijerumani la Abenzeitung kuwa imekuwa kawaida kwa timu zote duniani kufanya vitendo vya kupoteza muda zinapokuwa zinaongoza au kunufaika na matokeo yaliyo ubaoni na kuwa ilikuwa ni upumbavu kwa yeye kumsukuma kijana yule.
“Kila timu ina tabia ya kupoteza muda wakati mchezo ukiendelea hasa zikiwa nyumbani na matokeo yaliyopo kwa wakati huo yanainufaisha moja kwa moja kwakweli ilikuwa upumbavu kumsukuma(ball boy)
Bayern Munich wameondoshwa kwenye michuano ya UEFA Champions League baada ya kupata sare ya 2-2 kwenye mchezo huo na kufanya matokeo ya jumla kuwa 4-3 faida ya Inter Milan, Inter sasa watakutana na Vinara wa Laliga FC Barcelona April 30 mwaka huu.