EPL

‘Skipper’ achagua kubaki Liverpool

LIVERPOOL, Nahodha wa majogoo wa jiji Liverpool FC Virgil van Dijk amesema furaha anayoipata klabuni hapo ndio kishawishi kikuu cha yeye kuamua kuongeza mkataba wa kubaki klabuni hapo kwa miaka miwili zaidi wiki moja baada ya Mohamed Salah kuchukua uamuzi kama huo.

Tangazo la kuongeza mkataba la Virgil van Dijk linakuja wakati huu vinara hao wa EPL wakihesabu siku kabla ya kutangazwa rasmi kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England katika msimu wa kwanza wa kocha Arne Slot kikosini hapo

“Nina hisia mseto ambazo zinazunguka kichwani mwangu hivi sasa. Ni hisia ya kujivunia, ni hisia ya furaha. Ni hisia nzuri sana. Safari ambayo nimekuwa nayo hadi sasa imejaa furaha mara zote, kuweza kuongeza kwa miaka mingine miwili katika klabu hii ni hisia nzuri na nina furaha sana hapa bila shaka ningependa kuipata furaha hii.” Amesema Van Dijk

Van Dijk, 33, ameichezea Liverpool mechi 314, akifunga mabao 27. Ameshinda Ligi Kuu ya England, Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA, makombe mawili ya Carabao, Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu, yote chini ya meneja wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp.

Mwezi uliopita Van Dijk alisema “hajui” kama angesalia Anfield lakini Jumapili akadokeza kwamba alikuwa tayari kuongeza muda wake wa kukaa Anfield. Kusaini huku kunasitisha tetesi za jitasa hicho cha Kiholanzi kutimkia kwa vigogo wengine wa soka ikiwemo Real Madrid.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button