Nyumbani

Simba, Yanga kupigwa Novemba 5, 2023

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mechi ya watani wa jadi kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC itapigwa Novemba 5, 2023 saa 11:00 jioni katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo imetolewa leo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya Ligi Kuu.

Katika mechi za mzunguko wa kwanza kwenye msimu 2023/24, Simba itaanza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar, huku Yanga SC ikianza nyumbani dhidi ya KMC katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Related Articles

Back to top button