
TIMU ya Singida Fountain Gate imetangaza kufanya tamasha lake ‘SINGIDA BIG DAY Agosti 2, 2023.
Kwa sasa kikosi cha klabu hiyo kipo Karatu mkoani Arusha kikiendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano.
“Jiandae kufahamu kikosi chetu kamili cha msimu wa 2023/24 pamoja na burudani ya mechi kali ya kimataifa,” imesema taarifa ya klabu hiyo.
Mbali na kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Singida Fountain Gate pia itashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.