Mastaa

Shamsa Ford atoa ya Moyoni kuhusu ‘kupost’ mpenzi

Nisingeposti mpenzi, ningesubiri mume nimposti

DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu za Bongo, Shamsa Ford, ameibuka na ujumbe mzito wa funzo kwa mabinti, akitumia uzoefu wa maisha yake ya mahusiano kama somo kwa jamii.

Shamsa amesema kuwa kama angepata nafasi ya kurudisha nyuma miaka, asingeposti wala kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi alipokuwa bado hajaolewa, bali angemruhusu mume wake wa ndoa pekee kuwa mwanaume wa kwanza kufahamika hadharani.

Shamsa ameeleza kuvutiwa na namna mwigizaji mwenzake Jenipher Kyaka maarufu Odama anavyoyaishi mahusiano yake kwa usiri mkubwa, jambo alilolisifu kuwa ni mfano bora kwa mtoto wa kike.

Shamsa amesema anaonea “wivu wa maendeleo” nidhamu ya Odama katika kulinda faragha ya mapenzi yake, akisisitiza kuwa si kila jambo la moyo linapaswa kupelekwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Napenda sana jinsi unavyoyaweka mahusiano yako ‘private’. Sijawahi hata siku moja kukuona ukimpost boyfriend, na hicho ndicho kitu kizuri kwa mtoto wa kike, sio kila siku unampisti huyo mara ukiachana nae unamposti mwingine mkiachana unafuta ndo nini” amesema Shamsa.

Ameendelea kufunguka kwa kusema kuwa uzoefu wake wa zamani umemfundisha thamani ya faragha katika mapenzi, hasa kwa wanawake walioko kwenye macho ya umma.

“Kama ningerudisha siku nyuma, kipindi kile nilipokuwa single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yeyote niliyekuwa naye. Natamani mume wangu ndiye angekuwa mwanaume wa kwanza kwa watanzania kumjua,” ameongeza.

Kauli ya Shamsa imepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, huku wengi wakiona ni funzo lenye uzito kwa mabinti wanaokimbilia kuanika mahusiano yao hadharani bila kutafakari athari zake za muda mrefu.

Related Articles

Back to top button