Sevilla yamsajili kinda Nianzou akitokea Bayern

KLABU ya Sevilla ya Ligi Kuu ya Hispania imemsajili beki Tanguy Nianzou akitokea Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitano.
Nianzou raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ambaye alijiunga na Bayern akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2020 kwa uhamisho uhuru kwa kiasi kikubwa amekuwa mchezaji wa upande wa pembeni wa klabu hiyo.
Gazeti la michezo Bild la Ujerumani limeripoti kwamba Bayern itapokea ada ya Euro milioni 16 sawa na shilingi bilioni 37.5 ambazo zinaweza kuongezeka hadi Euro milioni 20 sawa na shilingi 46.8 pamoja na bonasi.
Nianzou amecheza michezo 28 katika misimu miwili akiwa Munich huku kwa kipindi kirefu akikaa benchi kutokana na majeraha na maambukizi ya virusi vya Korona.
Sevilla imekuwa ikitafuta beki mpya wa kati tangu kuondoka kwa Jules Kounde aliyejiunga na Barcelona.