Filamu

Serikali ya Uganda ndiyo iliyoiwezesha filamu ya ‘Iddi Amini

ZANZIBAR: FILAMU iliyofungua Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (ZIFF), ‘Janani: The Last Stand’ iliyomuhusisha Rais wa zamani wa Uganda Iddi Amini Dada na kasisi wa dini nchini humo imewezeshwa na serikali ya Uganda kwa lengo la kukumbuka maisha ya Askofu Mkuu Janani Luwum ambaye alitoa maisha yake kwa ajili ya wanyonge wa Uganda.

Hayo yameelezwa na aliyetengeneza sinema hiyo Matt Bish katika mkutano wake na waandishi wa habari kupitia mtandaoni yeye akiwa nchini Uganda.

Pamoja na kutotaja kiwango cha serikali ilichowezesha filamu hiyo kutengenezwa alisema kwamba sinema hiyo haimhusu Iddi Amini inamhusu Askofu huyo mkuu kwa lengo la kukumbuka moja ya mashujaa waliosaidia kukombolewa kwa Uganda toka kwa mikono ya iddi Amin.

Matt Bish ambaye mwenyewe hakuweza kufika katika onesho hilo mjini Zanzibar amesema amefurahishwa na kuwezeshwa kutengeneza sinema hiyo na kwamba amejitolea kuweka historia ngumu ya Uganda.

Filamu hiyo inayomzungumzia Askofu Mkuu Janani Luwum wakati wa kipindi kigumu cha historia ya Uganda wakati hofu ikikumba taifa hilo chini ya dikteta wa Idi Amin na mauaji ya wananchi ina kihoro kikubwa tangu inaanza mpaka inamalizika.

Askofu Mkuu Luwum nafasi iliyoigizwa na Peter Odeke, anaoneshwa katika nyakati zake za mwisho akilaani kwa ujasiri ukatili uliofanywa na utawala wa Amin upinzani ambao uligharimu uhai wake.

“’Janani: The Last Stand’ ni zaidi ya kipande cha sinema; ni chombo kinachobeba kumbukumbu za zamani zenye dhoruba, ambapo sauti za waliokandamizwa zilinyamazishwa, na hofumeeleza mmoja wa walioshuhudia filamu hiyo ikioneshwa kwenye skrini kubwa.

Related Articles

Back to top button