Kwingineko

Reina ‘kuvua glavu’ mwisho wa msimu

MILAN:GOLIKIPA wa zamani wa mabingwa wa ligi kuu ya England Liverpool na timu ya taifa ya Spain Pepe Reina ametangaza kuwa atastaafu soka msimu huu utakapofikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na kuhitimisha safari yake ya soka ya zaidi ya takriban miaka 24.

Reina ambaye ni zao la academy ya FC Barcelona alidumu na kujizolea umaarufu mkubwa alipokuwa katika ligi kuu ya England akiwatumikia vigogo Liverpool ambako alitwaa kombe la FA na Carabao Pamoja na mafanikio binafsi ya tuzo ya Golden Glove ya ligi kuu kwa kuwa na ‘Cleansheets’ nyingi katika misimu yake mitatu ya mwanzo klabuni hapo.

Ukiachana na FC Barcelona alikoanzia maisha ya soka, Nyanda huyo pia amezitumikia klabu mbalimbali kubwa ulimwenguni zikiwemo Bayern Munich, Napoli, Aston Villa, Lazio, Villareal na AC Milan kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Como mwezi July mwaka jana akicheza mechi 11 pekee msimu huu.

“Kazi yangu nzuri sana inakaribia mwisho, nimeishi maisha kamilifu sana. Ninajiona mwenye bahati sana kwa ambayo nimepitia. Sikutarajia, lakini nadhani wakati umefika na ninaona ni bora safari hii nzuri ikakomea hapa” amesema Reina katika mahojiano na Movistar
Reina ‘kuvua glavu’ mwisho wa msimu

MILAN, Golikipa wa zamani wa mabingwa wa ligi kuu ya England Liverpool na timu ya taifa ya Spain Pepe Reina ametangaza kuwa atastaafu soka msimu huu utakapofikia tamati mwishoni mwa mwezi huu na kuhitimisha safari yake ya soka ya zaidi ya takriban miaka 24.

Reina ambaye ni zao la academy ya FC Barcelona alidumu na kujizolea umaarufu mkubwa alipokuwa katika ligi kuu ya England akiwatumikia vigogo Liverpool ambako alitwaa kombe la FA na Carabao Pamoja na mafanikio binafsi ya tuzo ya Golden Glove ya ligi kuu kwa kuwa na ‘Cleansheets’ nyingi katika misimu yake mitatu ya mwanzo klabuni hapo.

Ukiachana na FC Barcelona alikoanzia maisha ya soka, Nyanda huyo pia amezitumikia klabu mbalimbali kubwa ulimwenguni zikiwemo Bayern Munich, Napoli, Aston Villa, Lazio, Villareal na AC Milan kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Como mwezi July mwaka jana akicheza mechi 11 pekee msimu huu.

“Kazi yangu nzuri sana inakaribia mwisho, nimeishi maisha kamilifu sana. Ninajiona mwenye bahati sana kwa ambayo nimepitia. Sikutarajia, lakini nadhani wakati umefika na ninaona ni bora safari hii nzuri ikakomea hapa” amesema Reina katika mahojiano na Movistar

Reina ambaye aliitumikia timu ya taifa ya Spain kwa michezo 36 amesema anatarajia kuutumia ujuzi wake ulioliwezesha taifa lake kuwa bingwa wa Dunia mwaka 2010 na bingwa wa Ulaya mwaka 2008 na 2012 kufundisha soka ili kukuza vipaji kama yeye.

Related Articles

Back to top button