
MICHEZO ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA inaanza leo kwa michezo 2 kupigwa Kigoma na Simiyu.
Katika mchezo wa Kigoma timu ya Kigoma Kwanza itavaana na Kakubilo ya Geita katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Katika mchezo wa pili Buhare ya Mara itakuwa mgeni wa Lamadi ya Simiyu katika uwanja wa Halmashauri, Simiyu.
Michezo mingine miwili ya awali ya FA itafanyika Novemba 6 ambapo timu ya Kibadeni ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Tandika United ya Dar es Salaam kwenye uwanja wa shule ya Minaki mkoani Pwani.
Nayo Kawele ya Kilimnjaro itakuwa mgeni wa Misitu ya Tanga katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga.