Muziki
Rais Samia ampatia Bitchuka Sh milioni 10

DAR ES SALAAM; Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemtembelea na kumjulia hali Mwanamuziki nguli nchini, Hassan Bitchuka nyumbani kwake Sinza Mori, jijini Dar es Salaam.
Mwana FA alimtembelea mwanamuziki huyo jana na kufikisha salamu kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan za kumtakia kila la heri na kumuombea afya njema apone haraka.
Aidha, Rais Samiaametoa kiasi cha Sh milioni 10 kwa mwanamuziki huyo kwa ajili ya kumtia moyo katika kipindi hiki cha matibabu.




