Paula ‘amuwekea fensi’ Marioo

DAR ES SALAAM: MSANII nyota wa Bongo Fleva, Omary Mwanga ‘Marioo’, amefichua namna mpenzi wake Paula Kajala anavyomjali katika suala la lishe, akisisitiza kuwa Paula hupenda amuone akiwa kwenye hali bora kiafya na kimwili.
Akizungumza hivi karibuni, Marioo amesema Paula ni miongoni mwa wanawake wanaojali afya za wapenzi wao na hawapendi waone wakila vyakula visivyo na tija kwa wanaume.
“Anapenda nile vyakula vinavyonipa nguvu, hasa katika kuongeza uwezo na ushupavu wa mwanaume,” amesema Marioo.
Kwa upande wake, Paula naye alithibitisha hilo amesema:“Mimi kama mama wa mtoto wake, sikubali ale chips mara kwa mara. Ni ugali kwenda mbele ili apate nguvu zaidi.”
Paula amesisitiza kuwa ni muhimu wanaume kula vyakula vyenye virutubisho na kuongeza nguvu, ikiwemo ugali, viazi vya kuchemsha, chapati, na vinginevyo vinavyosaidia kujenga mwili na kuimarisha afya kwa ujumla.




