FALigi Daraja La KwanzaLigi KuuNyumbaniU20

Nyota kibao kukutana Usiku wa Tuzo Moro Kids

NYOTA mbalimbali wanaosakata kandanda la kulipwa wanatarajiwa kukutana katika tukio la Usiku wa Tuzo za kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji ‘Moro kids’ ikiwa ni maadhimisho ya miaka 25 ya kituo hicho.

Akizungumza Leo Juni 20 Mratibu wa kituo hicho Rajabu Kindagule amesema siku hiyo kutakuwa na nyota mbalimbali waliopita katika kituo hicho na kufanikiwa kucheza timu ya taifa ambapo kutakuwa na tuzo za kuwapongeza kwa mafaniko waliyopata.

” Tutakuwa na mechi nyingi siku hiyo, Moro All Stars pia watakuwepo lengo letu ni kutaka kuonesha mafanikio tuliyoyapata” amesema Kindagule

Baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuwepo siku hiyo katika Viwanja vya sabasaba mjini Morogoro ni Mzamiru Yassin wa Simba, Kibwana Shomary, Dickson Job Abutwalib Mshery wote wa Yanga na Juma Abdul miongoni mwa wengine.

Related Articles

Back to top button