Kwingineko

Mwili wa Ssebo kuagwa Jumamosi

DAR ES SALAAM; MWILI wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Biashara wa kampuni ya E-Media, marehemu Denis Busulwa maarufu kama Ssebo, unatarajiwa kuagwa rasmi Jumamosi, Machi 14, 2026 katika viwanja vya Sanyansi vilivyopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Taarifa za ratiba ya mazishi zimetolewa na Mratibu wa Vipindi wa E-Media, Dizzo, ambaye amesema kwa sasa shughuli za maombolezo zinaendelea nyumbani kwa baba mlezi wa marehemu eneo la Mikocheni njia ya Rose Garden.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kufika kutoa pole na kushiriki katika msiba huo huku maandalizi ya shughuli za kuaga mwili yakiendelea.

Awali, taarifa za kifo cha Busulwa zilithibitishwa na Mkurugenzi wa E-Media, Francis Shiza maarufu kama Majizo.

Katika kipindi cha maombolezo, watu mbalimbali wakiwemo viongozi, wasanii pamoja na watu maarufu kutoka sekta tofauti wamekuwa wakifika nyumbani kwa familia ya marehemu kutoa heshima za mwisho na kuifariji familia.

Marehemu Busulwa alitambuliwa kama mmoja wa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia ya habari na biashara ya vyombo vya habari kupitia majukumu yake ndani ya E-Media.

Related Articles

Back to top button