Kwingineko

MwanaYouTube akamatwa kwa dawa za kulevya

MIAMI: MWANZILISHI wa mtandao wa YouTube, Jack Doherty, amekamatwa kwa mashtaka ya kumiliki dawa za kulevya na mashtaka mengineyo huko Miami.

Doherty, ambaye amejulikana kwa kuunda video za kejeli, alikamatwa wakati akirekodi video na kujaribu kuwasiliana na maofisa wa polisi katikati ya barabara, hali iliyozuia msongamano, kulingana na nyaraka za kukamatwa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani.

Polisi walimkamata Doherty kabla ya ukaguzi wa polisi kubaini kidonge nusu cha mviringo kilichokuwa na namba 3, kinacholingana na dawa ya aina ya amphetamine Schedule II, na sigara tatu zinazozaniwa kuwa ni bangi.

Doherty, mwenye umri wa miaka 22, anajulikana kwa kuandaa video za ujasiri zinazojumuisha kejeli, zikiwamo zile; “Niligonga gari la polisi.”

Doherty ana zaidi ya wanachama milioni 15 kwenye YouTube, wafuasi zaidi ya milioni 10 kwenye TikTok, na followers zaidi ya milioni 2.8 kwenye Instagram. Hakuna taarifa kama ana wakili wa kujitetea. Mwakilishi aliyeorodheshwa kwenye mitandao yake ya kijamii hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Doherty alihifadhiwa katika Kituo cha Mazeo ya Turner Guilford Knight, na mamlaka zimesema ana mashtaka kadhaa ikiwamo kumiliki dawa ya kusimamiwa, kumiliki bangi, na kupinga kukamatwa. Kukamatwa huku kunazidi kuonesha mfululizo wa migogoro inayomzunguka mwanaYouTube huyo, ambaye awali amekosolewa kwa kufanya stunts za umma zinazovuruga trafiki au kuleta taharuki kwa polisi.

Wataalamu wa sheria wamesema kumiliki dawa ya Schedule II bila cheti cha matibabu huko Florida ni jinai kubwa inayoweza kusababisha adhabu, kulingana na matokeo ya kesi na rekodi za makosa yaliyotangulia.

Licha ya matatizo ya kisheria, Doherty bado ni moja wa wanaharakati wenye ushawishi mkubwa mitandaoni, akiwa na mamilioni ya wafuasi wanaoshiriki kwa karibu na maudhui yake.

Related Articles

Back to top button