Ligi KuuNyumbani

Mwambusi kuwakata wachezaji mishahara ya Nov.

KOCHA Mkuu wa Ihefu, Juma Mwambusi amesema anafikiria kuwakata mishahara ya Novemba, 2022 baadhi ya wachezaji walioshindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo na kusababisha kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Ihefu ilipoteza mchezo huo uwanja wake wa nyumbani Highland Estates kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Polisi Tanzania Novemba 17, 2022.

“Uongozi umewekeza pesa nyingi na bado umeonesha uvumilivu mkubwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha sasa kuendelea kufanya makosa ambayo yanaigharimu timu ni kosa kubwa kwenye ligi yenye ushindani kama hii,” amesema Mwambusi.

Amesema makosa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara kwenye mechi za timu hiyo ingawa yeye na wenzake benchi la ufundi wamekuwa wakijitahidi kurekebisha hali hiyo lakini imekuwa ngumu kupata ushindi.

Ihefu ambayo imepanda msimu huu kutoka Championship kwa sasa inashika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano huku ikishikilia rekodi ya kupoteza michezo minne iliyopita.

Related Articles

Back to top button