Kwingineko

Mokwena ‘mikono juu’ Wydad

CASABLANCA: KOCHA wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates za South Africa Rulani Mokwena ameondoka katika klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco baada ya kudumu kwa miezi 9 kufuatia matokeo mabaya ya klabu hiyo yenye jina kubwa kwenye soka la Africa

Mokwena kocha kijana mwenye miaka 38 alitua Wydad baada ya kutimuliwa na Mamelodi Sundowns mwisho wa msimu uliopita licha ya kuwaweka masandawana kwenye kilele cha ligi kuu ya South Africa (Betway Premiership) na kuwapeleka kwenye fainali ya kombe la ligi (Nedbank Cup) na nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Africa (CAFCC).

Kuondoka kwa Mokwena bado hakujatangazwa rasmi na Wydad lakini ni Habari ya ukurasa wa mbele kwenye gazeti la michezo la Morocco la Al Mountakhab. Mokwena bado ana mkataba na klabu baada ya kusaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo hado 2027 lakini mapema mwezi huu alitangaza kuondoka mwishoni mwa msimu.

Habari zaidi zinasema kuwa kuharakisha kuondoka kwake ni kufuatia sare sita mfululizo kwenye ligi kuu nchini Morocco Botola Pro League matokeo yalioifanya Wydad iongeze pengo la pointi hadi 6 nyuma ya walio nafasi ya pili klabu ya Royal Armed Forces ikiwa hatihati kuikosa ligi ya mabingwa msimu ujao Pamoja na kuondolewa katika hatua ya 16 bora ya Throne Cup na klabu ya Mohgreb Tetotuan.

Kuondoka kwa Mokwena kuna maana kuwa hatavaa jezi ya klabu hiyo kwenye kombe la dunia la klabu litakalofanyika nchini Marekani mwezi Juni mwaka huu ambako angeweza kukutana uwanjani na ‘role model’ wake Pep Guardiola wa Manchester City.

Related Articles

Back to top button