KLABU ya Dodoma Jiji imemteua Melis Medo kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.
Taarifa ya Dodoma Jiji imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Masoud Djuma.
“Uongozi unawaomba mashabiki wetu na wapenda michezo wote kumpa ushirikiano wa kutosha kocha Medo katika kipindi chote atakachohudumu kama mkuu wa benchi la ufundi,” imesema taarifa.
Medo alikuwa kocha wa Coastal Union kabla ya kutimuliwa Februari, 2022 kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
Oktoba 10,2022 Dodoma Jiji ulifikia makubaliano ya pande zote mbili kutoendelea na Kocha Masoud Djuma.



